Showing posts with label Trainings. Show all posts

KARIBU YEMCO


MAFUNZO YA WALIMU WA VICOBA

 

Katika kuendeleza harakati za kufundisha Walimu ambao watakuwa tayari kwa ajili ya kutoa elimu ya mfumo Wa Vicoba Endelevu Tanzania,Taasisi ya Youth Empowerment and Mindset Change Organization(YEMCO) imeanza rasmi mafunzo hayo leo tarehe 8/05/2017 na yanatarajiwa kufikia kikomo tarehe 11/05/2017..




Akizungumza na waalimu hao wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mohamed Bassanga Mkurugenzi wa taasisi ya YEMCO amewasisitizia walimu hao wa VICOBA kusimamia sheria na taratibu za uendeshaji wa vikundi endelevu vya VICOBA na kuepuka kufanya udanganyifu wowote kwani serikali imetilia mkazo juu ya sheria hizo










inatangaza kuanza usajili Wa mafunzo ya Walimu Wa Vicoba awamu ya tatu.Mafunzo yatafanyika tar 15-18/5/2017 kuanzia SAA NNE kamili hadi SAA kumi jioni.Makao makuu ya YEMCO-Sinza white inn.

MAFUNZO KWA MABALOZI WA YEMCO




Mabalozi wa kujitolea wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa YEMCO



Tarehe 17/5/2017 imeingia katika vitabu vya kumbukumbu vya taasisi inayojihusisha na kuwawezesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu YEMCO baada ya kuanza rasmi kutoa mafunzo kwa vijana 10 ambao wamechaguliwa kuwa mabalozi wa kujitolea kwa taasisi hiyo.

Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa taasisi ya YEMCO Mh. Mohamed Bassanga amewakaribisha vijana hao ambao ni mabalozi na kuwashauri kuitumia nafasi waliyoipata kuwaelimisha vijana wengine ambao wapo nje ya taasisi maalumu kama taasisi za elimu.



Mabalozi wakifuatilia kwa umakini mafunzo.



Akizingumza na vijana hao Afisa miradi wa taasisi yetu Ndugu Justus August amewashauri vijana  kuwa kuna umuhimu wa kujitolea kama njia ya kujiongezea uzoefu na kujuana na watu mbalimbali. Licha ya yote Justus amewasisitizia kuwa baada ya leo ni jukumu la mabalozi hao kuhakikisha kila palipo na mkusanyiko wa watu kumi kati yao nane wawe wanaitambua taasisi ya YEMCO.

Afisa Uchechemuzi wa taasisi ya YEMCO Bi Nyangoub Nyamsogoro.


Baada ya mafunzo hayo washiriki walipata nafasi ya kushiriki kwenye mdahalo wa pamoja uliolenga kwenye kuelezea faida za kujitolea. Mdahalo huo ulifanyika katika mtandao wa tweeter na unaweza kuufuatilia kupitia akaunti ya tweeter @YEMCOTanzania ama kupitia  #Faidazakujitolea. 




KIJANA JITAMBUE NA UJIAJIRI PROJECT

Kijana jitambue ujiajiri is among of our project which we did with youth from diferent part of the Tanzania