YEMCO AMBASSADOR

May 15, 2017 Unknown 0 Comments



Taasisi inayojihusisha na kuwainua vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kiuchumi na kubadilisha mtazamo, inatoa taarifa kwa ajili ya zoezi la kutafuta mabalozi wa taasisi hiyo kuwa fomu zote za walioomba nafasi ya kuwa mabalozi zimeshapitiwa na utaratibu wa kuwatangaza waliofanikiwa kupata nafasi hiyo utafanyika hivi punde.

Hivyo taasisi yetu inawasihi vijana wote walio vyuo vikuu ama nje ya taasisi za elimu kuwa na subra na kuendelea kutufuatilia kwa ukaribu kupitia mitandao yetu ya kijamii kuweza kupata taarifa sahihi pindi zinapotoka.

0 comments: