MAFUNZO KWA MABALOZI WA YEMCO

May 17, 2017 Unknown 1 Comments




Mabalozi wa kujitolea wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa YEMCO



Tarehe 17/5/2017 imeingia katika vitabu vya kumbukumbu vya taasisi inayojihusisha na kuwawezesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu YEMCO baada ya kuanza rasmi kutoa mafunzo kwa vijana 10 ambao wamechaguliwa kuwa mabalozi wa kujitolea kwa taasisi hiyo.

Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa taasisi ya YEMCO Mh. Mohamed Bassanga amewakaribisha vijana hao ambao ni mabalozi na kuwashauri kuitumia nafasi waliyoipata kuwaelimisha vijana wengine ambao wapo nje ya taasisi maalumu kama taasisi za elimu.



Mabalozi wakifuatilia kwa umakini mafunzo.



Akizingumza na vijana hao Afisa miradi wa taasisi yetu Ndugu Justus August amewashauri vijana  kuwa kuna umuhimu wa kujitolea kama njia ya kujiongezea uzoefu na kujuana na watu mbalimbali. Licha ya yote Justus amewasisitizia kuwa baada ya leo ni jukumu la mabalozi hao kuhakikisha kila palipo na mkusanyiko wa watu kumi kati yao nane wawe wanaitambua taasisi ya YEMCO.

Afisa Uchechemuzi wa taasisi ya YEMCO Bi Nyangoub Nyamsogoro.


Baada ya mafunzo hayo washiriki walipata nafasi ya kushiriki kwenye mdahalo wa pamoja uliolenga kwenye kuelezea faida za kujitolea. Mdahalo huo ulifanyika katika mtandao wa tweeter na unaweza kuufuatilia kupitia akaunti ya tweeter @YEMCOTanzania ama kupitia  #Faidazakujitolea. 




1 comment:

  1. Nahitaji kujitolewa katika organization yenu ili nipate uzoefu kwa vitendo, nimemaliza chuo kikuu cha kilimo cha sokoine yaani sua.
    Uhandisi wa kilimo..nawezaje kupata hiyo nafasi?

    +255769120116 Ezra Kayanda.

    ReplyDelete